MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19)
Habari Watanzania wenzangu!!
Naitwa Amiry Kaiza, mwanaharakati na mbobezi katika kuelimisha jamii.
Leo niko hapa kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania wenzangu wa rika zote katika kupambana na ugonjwa hatari wa homa ya mapafu yaani Corona. Kama mnavyojua ugonjwa huu tayari umesababisha vifo zaidi ya 50,000 duniani kote na tayari zaidi ya watu 1,000,000 wameambukizwa ugonjwa huu. Sisi kama Watanzania tunaweza kusaidia serikali katika kusambaza elimu kwa jamii ili kuepuka madhara makubwa ya ugonjwa huu.
Kama unaunga mkono kampeni hii naomba tufanye maadhimio kufanya yafuatayo:
1. Kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona kwa kuzingatia taarifa rasmi zinazotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).
2. Kuwasaidia watu wenye ulemevu wa viungo vya mwili kama vipofu. Kwasababu watu hawa wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu kutokana na kuhitaji msaada wa kushikwa mkono pale wanapohitaji kuongozwa njia kitendo kinachoweza kupelekea kuambukizwa.
3.Kufuata kanuni na maelekezo ya nayotolewa na Wizara ya Afya kama kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka misongamano, kuacha kushikana mikono, kubusiana, kukumbatiana na kuepuka safari zisizo za lazima.
4. Kutoa taarifa zilizo sahihi zinazotolewa na Wizara ya Afya, Waziri mkuu, Waziri wa Afya, Msemaji mkuu wa serikali pamoja na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuacha kutoa taarifa za uongo au uzushi unaoweza kusababisha taharuki katika jamii.
Mimi naipenda nchi yangu ndiyo maana nawekeza nguvu zangu katika kuelimisha jamii, WEWE JEEE??!!!!!
Naomba ujisajili kwa kuandika jina lako,email pamoja na sababu ya kuunga kampeni hii hapo chini ili kuonesha jinsi gani unaunga mkono juhudi hizi
Kwa mawasiliano:
amiryabdallah@gmail.com
Amiry Abdallah Kaiza Contact the author of the petition
Announcement from the administrator of this websiteWe have closed this petition and we have removed signatories' personal information.European Union's General Data Protection Regulation (GDPR) requires a legitimate reason for storing personal information and that the information be stored for the shortest time possible. |